Saturday, April 25, 2009

HEKA HEKA ZA ANGUKO LA FEDHA KATIKA MAREKANI NA UCHUMI WA TANZANIA

UKWELI ULIFICHWA NA WANASIASA NCHINI LAKINI UKWELI WA MAMBO ANGUKO LA BISHARA YA FEDHA KATIKA MAREKANI(USA) LINA MADHARA KATIKA UCHUMI WA ULIMWENGU,TANZANIA IKIWEMO.
TATIZO LA SASA HIVI LIMESABABISHWA NA AGUKO LA BIASHARA YA FEDHA LILILOPELEKEA ANGUJO LA KIUCHUMI.
FAHAMU CHANZO CHAKE,MADHARA YAKE KWA TANZANIA NA NINI TANZANIA IFANYE
FUATILIA MFULULIZO HUU WA MAKALA HII ITAKAYOTOKA KARIBUNI.

ETI DECI TISHIO!!!!

ETI DECI LILIKUWA TISHIO KWA ASASI ZA FEDHA!kUNA WAANDISHI WAKONGWE NAONA WANAFUATA MANENO YALE YALE YA KISWAHILI KUWA NGOMA IKILIA SANA MWISHO UPASUKA. hILI LINADHIHIRIKA KATIKA HOJA ZAO. KUPITIA KURASA ZA MAGAZETI MBALIMBALI NA KWA VILE WANA NAFASI ZAO 'COLUMN' MARA NYINGI WANAJIKUTA WANINGIA KATIKA VITU AMBAVYO HATA HAVINA UKWELI HATA CHEMBE.
LABDA KWA VILE HAWANA UELEWA NA MAMBO YA BIASHARA, NASEMA LABDA LAKINI TUSISAHAU KUWA KUKOSA UFAHAMU NA JAMBO HUSIKA HALIKUZUII WEWE KUSOMA AU KUJIFUNZA. LILILOWAZI NI KWAMBA WAKONGWE HAWAFUNGUI MAKABRASHA.
NASEMA WAKONGWE KWA VILE SIKUTEGEMEA HOJA HII INGEUNGWA MKONO NAO.'DECI TISHIO TOKA LINI'
TANZANIA INAKADIRIWA KUWA NA BENKI ZAIDI YA 40, ACHILIA MBALI WATOA MIKOPO KAM BAY PORT,PRIDE NA BLUE FINANCIAL SERVICES KWA KUTAJA TAASISI CHACHE TU.
PAMOJA NA UKUAJI HUU ULIOIBUKA MIAKA YA 9O KULIKOCHANGIWA NA MABADILIKO YA KIUCHUMI NCHINI BADO MABENKI HAYA YAMEWEZA KUFIKIA WATEJA 10% TU YA WATU WANAKADIRIA KUFIKIA MILIONI 40 WA CHI HII.
BADO KATIKA TANZANIA BENKI YOYOTE INWEZA KUJA NA KUPATA WATEJA KWANI SOKO LIPO. tUNA BENKI ZINZPATA FAIDA ZIKIWA BADO ZINAFANYA BIASHARA KWA KUHUDUMIA WATEJA WAKUBWA 'CORPORATE CUSTOMER'
RETAIL KWAO NI KAMA MZIGO KWA VILE GHARAMA ZA KUTOA HUDUMA KWA RETAIL NI HASARA TUPU KWAO....
MAKALA HII INAKUJA FUATILIA.

Monday, April 20, 2009

Kupambana na umasikini sawa ila njia tunazotumia si sahihi

Profesa Fernando De Sotto gwiji wa uchumi mdogo (Micro economics) kutoka Peru katika kitabu chake cha ‘The other path’ anaandika ‘mifumo mibovu ya uchumi uzalisha vyanzo vya kipato visivyo halali’ Kitabu hiki kilitokana na tafiti yake aliyoifanya Peru. Peru ni sawa na Tanzania ina mashaka yanayofanana nasi ingawa mazingira yetu ya kijiografia yanatofautina ila lililowazi nikwamba mifumo mibovu ya uchumi inayoinyonga Peru ndiyo hiyo hiyo inayoinyonga Tanzania.

Nimeona vema nianze na nukuu ya gwiji huyu ili kuweka bayana kuwa upatu kwa naman oyoyte ni matunda ya uchumi wenye mifumo kandamizi, na isieleweke hata kidogo kuwa kutokana na kuchipuka kwa vikundi hivyo vya ujanja ujanja kuna mwisho mwema miongoni mwa washiriki.

Katika mazingira kama haya ya kuona riziki inaweza kupatikana kwa kujifanyia mambo ya kupora haki za waliowengi kwa njia za ujanja ujanja mara zote huonekana kama ndiyo tija ya watu wachache. Mara nyingi tulio masikini tumekuwa hatujifunzi jambo kutoka na na aina hizi za udanganyifu za kupata mafanikio kwa pupa.

Lazima ieleke kwamba Serikali yoyote Duniani jukumu lake kubwa ni kulinda haki za watu wake na si kuona kila wakati tunanyanyasika na kupokonywa hata kile kidogo tulichonacho. Mara zote masikini wamekuwa wagumu labda hili linatokana na hali yetu na kufikia kuona kuwa ‘liwalo na liwe’.

Mwaka 2007, tulijionea jinsi wajanja wachahce walivyo jipatia utajiri kupita michezo hii ya upatu. Tulipokuwa shule rafiki yangu alikuja na fomu ya kampuni ya ‘Faidika Investment’ na kunishauri kununua fomu ile kwa elfu 50,000/=. Nami baada ya mzunguko nitapata nafasi ya kupata fomu zangu tano zitakazopelekea kupata 250,000/=.

Uhakika wa fedha zangu kurudi itategemea sana na jinsi nitakvyoweza kushawihsi wengine kujiunga kwa kununa fomu yenye majina matano kwa shilingi elfu hamsini. Nilisita na kumwambia wazi kuwa asimuambie mtu kwani ameshaibiwa, huo ni upatu hauna mwisho mwema.

Kwa vile tulizoea kuwa na mijadala alihisi kuwa ndiyo chochoko zangu za mijadala zimeanza,akanishawishi kuwa huu si upatu kwani unachezeshwa na waumini wa kilokole wa EAGT ambalo yeye ni muuni wake. Nilijibu ulimwengu wa pesa mgumu hauna mlokole wala aliye karibu na madhabahu angalia unaibiwa, nilisisitiza.

Miaka miwili leo hii tangu FAIDA isimamishwe na mkurugenzi wake kufikishwa mahakamani ambaye alikuwa raia wa Kenya, sijui nini kiliendelea , ila yeye alipoteza shilingi 100,000 mpaka leo hajui aingilie ofisi gani ili kudai haki yake.Huo ndiyo upatu hauna mwisho mwema.

Nipo kibaruani mfanyakazi mwenzangu anakuja akitamba kuwa ana taarifa za mafanikio nazo kuhusu DECI akinimabia yeye amepanda 200,000/=. Nilimuambia nyamaza utachekwa ukweli wa mambo umeibiwa huo ni upatu, hauna mwisho mwema. Kitaaluma huyu ni mtaalamu wa Uchumi nilimtania kuwa kwa nadharia za biashara ulizosoma darasani ni lini ulipoambiwa kuwa mtaji unaweza kuleta faida ya asilimia zaidi ya 20 tena baada ya kulipa kodi nayo ikawa ni biashara halali kama si utapeli ni nini?

Liliowazi ni kwamba haya matukio ya FAIDA na DECI yanayahusisha makanisa ya uhamsho na yanatia ndani hulka ya pupa. Wakati umefika wa kuchambua mambo kwa kina na uwazi juu ya baadhi yetu tunaotumia kivuli cha madhabahu kuendesha dhuluma.Taasisi zenye dhamana ya kulinda usalama wanchi zichunguze kwa kina makanisa haya ya uhamsho.

Niliwahi kuandika katika siku za nyuma (2006) katika gazeti hili juu ya kushamiri kwa ‘pupa’ miongoni mwa watanzania kunakodhihirisha na kuibuka kwa michezo ya kamari nchini.

Pupa mara zote ikitawala hata uambiwe nini husikii, Naomba ielekwe bwana wa pupa ni shetani yule muovu.Faida investment imekuja imekula fedha za watanzania kwa kutumia ‘pyramid’ imeondoka leo hii tunashauriwa kuikubali DECI. Hii nini!Hatushangai kuona watanzania hawajakoma kwani hii ni kawaida yetu na hasa kwa vile pupa imekua ndiyo nguzo yetu ya maisha siku hizi. Chukulia mfano wa mchezo wa karata tatu unavyoumiza watu lakini bado utawaona wanang’ang’ania kucheza.

Naomba ieleweke kuwa kinachogomba si kwamba DECI haiwezi kuleta unafuu wa maisha kwa watanzania tuliowengi, wala si kwamba haiwezi kutoa mihela kwa watu waliowanyonge baada ya kukosa mikopo toka benki. La hasha isipokuwa ni kwamba njia inayotumiwa si halali ni njia ambayo kwa miaka mingi na matukio mbalimbali nchini imethibitisha ni utapeli mtupu.

Chumo la DECI asili yake wapi? Taasisi yoyote inafanya biashara ya fedha inatoa chumo lake kubwa toka katika mikopo na marejesho yanayotokana na mikopo kama riba ili kuendesha taasisi husika. Pia inaweza kupata fedha toka katika uwekezaji katika taasisi au shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile ununuzi wa hisa katika kampuni au hata benki na ununuzi wa dhamana za serikali.

Sasa chumo la DECI asili yake wapi, linalofanya kuweka 200,000 upate 500,000 ndani ya miezi mitatu. Nadharia za biashara zinabainisha wazi kuwa hakuna faida halali inayozidi asilimia 20. Nilitegemea menejimenti ya DECI ingeweka wazi sikuile PTA kuwa sisi tunaweza kutoa laki tano kwa mtu aliyetupa laki mbili kwa sababu ‘pando’ la mteja linawekezwa kwa jinsi hii nasi tunapata faida .

Lakini haikufanya hivyo ila ilikuja na hoja ya kuwa wao wanabinywa kwa vile kuna udini. Hii hoja si hai, ni kuishiwa kutoa hoja zinazojenga. Wanaendelea kutoa kilio kwa Rais Kikwete awatetee, sasa atetee nini? Taasisi gani inayoweza kuendeshwa kwa michango ya wanachama, eti inawanachama 600000 na kila mwaka wanachangia elfu 30, nasi tunajipatia bilioni 18, hivyo kwa pato hili sisi hatuwezi kutetereka!
Huku ni kuishiwa hoja walipaswa pia watuambie kuwa wakipata bilioni 18 wao wanazifanyia nini ili zikue,na hao wateja wasipokuja kinatokea nini?Au wanajifanya hawajui mzunguko wa biashara (business cycle) kuwa kuna siku utakuwa kileleni(Peak) kuna kipindi kutakuwa na ‘anguko’(recession)!

Gazeti la jumapili la mwananchi la tarehe 12.04.2009 lina taarifa ya mtu mmoja anayekiri kupata mafanikio kutokana na DECI pia anaeleza wazi kuwa kuna mtanzania ameweka zaidi ya milioni mia moja. Tuulizane DECI inafahamau kuwa kuna kitu kinaitwa ‘kuosha fedha’. Katika fedha zaidi ya trilioni moja (kama ilivyoripotiwa na gazeti moja la kila siku) ambazo inazo katika akaunti yake ni kiasi gani ni fedha halali?

Wakilili na Mhadhiri wa Chuo cha IFM, Eugene Mniwasa katika kazi yake ya ‘Detection and suppression of money laundering in Tanzania ; alivitaja vyanzo ambavyo vinapelekea mapato ya fedha haramu kuwa ni pamoja na mikopo isiyo rasmi. Sasa tujiulize katika shughuli hizi zinazofanywa na asasi hii ni kwa kiasi gani imechochea uoshaji wa fedha haramu. Menejimenti ya DECI inapaswa itujibu.

Sheria ya 2004 ya udhibiti wa fedha haramu pamoja na mambo mengine inataja juu ya kumtambua mteja (Customer identification) kabla ya kupewa huduma ya kufunguliwa akaunti sasa hawa jamaa wanakopeshana kwa kufungua kwa kiasi kidogo dogo kitu ambacho ni hatari, hii ni mbinu ya kusafisha fedha kati ya zile nyingi hii inaitwa layering (utagaji).

Muosha pesa huwa anakuwa na akaunti zaidi ya moja katika benki moja na anaweka kiasi kidogo kidogo ili asijulikane kiurahisi kuwa anachanzo cha chumo lisilo halali. DECI inawezekana bila kulitambua hili imejikuta inawezesha uoshaji wa fedha haramu.

Tanzania ni yetu sote lazima tulindane kwa kuhakikisha chumo halali linapatikana kwa kila mmoja wetu, ni wazi kuwa kuna kipindi waliowengi wanaweza kuona wanaonewa. Ila ifahamike kwamba umasikini wetu hauwezi kupunguzwa kwa kutetea kamari. Hatuna kinyongo na harakati zozote za kupunguza umasikini, ila zifuate njia za halali na si ujanja ujanja.

Kimsingi serikali inapaswa kulinda mali za watu wake, basi jicho la kumulika taasisi za mikopo ya fedha isiyo rasmi lazima liangaze kila kona ya nchi kwani DECI ziponyingi na kwa kutumia mwanya huo fedha haramu zinaoshwa kiurahisi kabisa.

Prince Niccollo Machiavelli aliwahi kubainisha wazi kwamba ‘raia anaweza kusahau na kukusamehe hata ukimuua babake lakini si kupora mali yake’Taarifa ya habari ya TBC1 14.04.2009, usiku saa imeripoti kadhia aliyoipata ofisa wa DECI maeneo ya mabibo pale wanachama walipogomba asitoke hadi polisi walipokuja kumuokoa,na taarifa zinasema Kenya waliuana mambo hayo hayo ya upatu, niwazi kuwa maneno ya Niccolo yana ukweli.

Shime wenye mamlaka,tekelezeni wajibu wenu na si kuona mambo yanaenda hovyo mnakaa kimya, kwani DECI iliomba kuwa SACCOS sasa mlikuwa munasubiri nini wakati mnaona kila kitu hakiendi sawa, au kwa vile ni walokole?Hii siyo sawa.

Kila mmoja wetu na atambue pupa haina mwisho mwema acha kucheza kamari. Mwenye masikio na asikie.

TURUDI VIJIJINI

NAINGIA LIBRARY KUJISOMEA.MBELE YANGU KUNA KIBAO KINATANGAZO JUU YA MEZA LINALOSOMEKA KWA KIMOMBO "DON'T RESHELVE BOOKS ON YOUR OWN.LEAVE THEM ON THE TABLE" NINA AMINI KIMOMBO UNAKINYAKA NA KAMA HAUKINYIKI NASEMA RUDI DARASANI KWANI SI VIBAYA.
JUU YA TANGAZO HILO KUNA MWINGINE ANALETA UTUNDU,ANAANDIKA MANENO YAKE,YAPO KWA KISWAHILI"BY BPA III HRM" KIREFU CHAKE NI BACHELOR OF PUBLIC ADMINISTRATION WITH OPTION IN HUMAN RESOURCE MANAGEMENT.MUNGU AMBARIKI AWEZE KUKWAPUA GAMBA LAKE;KWANI MUZIKI HUU SI WA KITOTO,QMS INASUMBUA KWELI.
NAANGALIA VIZURI MWINGINE ANAFANYA UTUNDU JUU YA LILE TANGAZO HUYU ANAANDIKA"SOMA URUDI KIJIJINI UKAWE KATIBU KATA".HE YAMEKUWA HAYO TENA!
HUYU WA PILI ANAYEANDIKA SOMA URUDI KIJIJINI NDIYE ANAYE NISUKUMA MPAKA ANANIFANYA NIHOJI ILI NIJUE NAWE UNAMTAZAMO GANI.INGAWA WOTE NI JEURI KWA KUANDIKA JUU YA MATANGAZO,HUKU NI KUKOSA NIDHAMU,HAINA UBISHI.
NAAMINI UNAOMA KWA MAENDELEO YA NCHI YAKO,AMBAYO WATU WAKE WENGI NI MASKINI,SISI TUKIWEMO.MIONGONI MWA MASIKINI HAO WAPO VIJIJINI,NA NDIO WANAMINYWA KWA KUTOZWA KODI NA SERIKALI ZA MAZAO ILI SISI TUSOMEMESHWE .
NATAMBUA WENGI WAO WANA MATUMAINI SIKU TUMALIZE MASOMO YETU ILI TUKAWE CHACHU YA MAENDELEO YAO.
KWENDA MAENEO YA MASHAMBANI WENGI WENU MUNAONA NI KUCHAKAA,NA KUISHIWA KWA MIPANGO.MUNATAMANI MUKAE MIJINI.HUKU WAKULIMA WA TANZANIA WAKIWA HAWANA NAMNA YAKUNG'OKA KUTOKA KWENYE LINDI LA UMASIKINI.MATUMINI YAO YAMEGEUKA MATESO KWAO,HAWANA WASOMI WAKUENDESHA USHIRIKA WAO;YAANI WAMEKATA TAMAA.WASOMI WA KILIMO MUPO MIJINI,WAKULIMA WAKIWA HAWANA VIONGOZI.
HAPA NAKUBALIANA NA MANENO YA PROFESA RENE DUMONTE,ALIYE WAHI KUSEMA AFRIKA INAKWENDA KOMBO KWA SABABU WASOMI WAKE HAWATAKI KURUDI MASHAMBANI,KUPELEKA CHECHE ZA MAENDELEO.MIAKA ZAIDI YA 25 IMEPITA TANGU MFARANSA HUYU KUANDIKA HIVI KATIKA KITABU CHAKE AFRIKA INAKWENDA KOMBO.
LAKINI BADO MANENO HAYO YANA UKWELI,LEO HII KWA UJUMLA WASOMI HATUTAKI KURUDI MAENEO YA MASHAMBANI.SHULE ZINAKOSA WALIMU;ZAHANATI HAZINA WAHUDUMU HUKU VIJANA TULIOSOMESHWA NA KODI ZA WAKULIMA,TUNATANGATANGA KATIKA MITAA YA MIJI MIKUBWA BILA KUTUMIA UTAALAMU WETU KAMA AHSANTE YETU KWA WALIPA KODI WA NCHI HII.FUNGUA MACHO NG'AMUA UKWELI,"AMBAO WAONYESHA WAZI KWAMBA MAENDELEO YA TANZANIA YATALETWA NA WATANZANIA WENYEWE KWA KUKUBALI KUITUMIKIA NCHI YAO KATIKA MAZINGIRA YA MASHAMBANI NA SI,MISAADA YA IMF,WB,EU WALA WAHISANI WA AINA YOYOTE ILE"
MIAKA YA 1960 VIJANA 400 WA CUBA,KUTOKA CHUO KIKUU CHA HAVANA,WAKIWA WAMEPEWA HOTELI YA KITALII YA RIVIERA NA KAZI KATIKA JIJI LA HAVANA,WALIGOMA WAKIDAI WAPANGIWE KAZI MAENEO YA MASHAMBANI.HII NI CHANGAMOTO KWETU SISI.TULIO CHINI KIMAENDELEO.
VIJANA WASOMI WA TANZANIA LEO HII HAWAKO TAYARI KURUDI, (HATA WALE WALISOMA SHAHADA ZA MAENDEO VIJIJINI BA.RURAL!!!!) KIJIJINI HUKU TUKILALAMA KUDAI KUONEWA NA MAOVU YA UKOLONI.
NDIYO.LAKINI HATA MAONI YAKO YAWE NINI,UKOLONI ULIOVICHWANI MWETU NI MBAYA ZAIDI,KULIKO MINYORORO YA KINA VON ZELEWISKY,KARL PETERS NA WENGINE.TUJIFUNGE KIBWEBWE KWA KUBEBA MSALABA WETU NA LAWAMA ZA UMASIKINI WETU,KAMA WATU AMBAO HATUKUWAJIBIKA KIPINDI KIREFU KWA WATU WETU.
SASA TWENDE TUKAPIGANIE MAENDELEO YA WENGI;KAMA VILE VIJANA WA UCHINA NA CUBA WAFANYAVYO.

Gwaride si njia sahihi ya kuleta uzalendo ila matendo ya watawala

Nimesikia na ninaamini umeshawahi kusikia watu wakieleza au kwa ukali au upendo neno "uzalendo".Imefikia hatua wengine katika mzungumzo ya kawaida kuwaita wenzi wao ni wa-zalendo au si wa-zalendo.Mimi najiuliza "uzalendo" ni nini?Mzalendo ni nani ?Ufanye nini ili uwe mzalendo?
Hata hao wanao wavua wenzao huo uzalendo,mara nyingi huwa hawana tafsiri isiyo na utata juu ya neno hili,uzalendo!Inashangaza sana.Ukiangalia sana kuna watu wengi,tia ndani wasomi ambao kwa wakati tofauti,wanaulezea huo uzalendo kama ni "hali".Hapa wanajenga picha ya kufikirika tu,au ni dhana tu ambayo inaweza kutofautiana kwa mchango wa mazingira yanayo mzunguka mtu mmoja toka sehemu moja hadi nyingine.
Kama tukikubali uzalendo ni hali,ni vipi sasa tunafamu mtu fulana ameikosa hiyo hali?Kwangu mimi vitendo hunena,basi matendo huonesha hali ya mtu kuelekea uzalendo,kama hivyo ndivyo basi,nakubali kwa dhati sasa kuingia kwenye "swimming pool" yenye maji kwa kujaribu kutoa tafsiri ya uzalendo.
'Uzalendo' ni ile hali ambayo binadamu anaihisi juu ya mashaka,taabu,shida,sononeko,hofu,madhara,inayo msibu yeye au mwenziwe,na binadamu hao kuwa na nia,malengo na makusudio ya kupambana na hali hiyo kandamizi kwa "gharama" sahihi kupelekea ushindi-dumu.sasa kama msingi mkubwa wa uzalendo ni mapambano sahihi,ili kupelekea faraja kwa walio na hali dhalili,je Afrika kuna wazalendo wa-kweli?
Dhana nyingine kubwa inayo jificha nyuma ya uzalendo ni mabadiliko,kuhusu mabadiliko,uzalendo unaamini ili mabadiliko yawe ya kizalendo lazima yawafaidi watu wengi hasa wa tabaka la chini,nao ni "wakulima"je mabadiliko ya kiuchumi na kijamii na kisiasa yanato tokea tanzania ni ya kizalendo?
Kuna wanao dai,kizazi cha sasa hasa walio zaliwa kuanzia miaka ya 1980,kimekosa uzalendo!Miradji mwandishi wa makala katika kona ya Darubini ya jumapili katika gazeti la majira la tarehe 26/9/03,anaunga mkono wazo kwamba kizazi cha sasa hakina uzalendo.
Kibubusa kabisa anasema JKT lirudishwe ili kurejesha huo uzalendo!je uzalendo ni kupiga "kwata".hata kidogo.
Nimeshaandika kwamba dhana ya uzalendo inaenda sambamba na mazingira,kwa mfano kwa nchi ya marekani,vita ni njia moja wapo ya kuonesha fulani ni mzalendo.wapinzani wa bush jr,walidai wazi kabisa kwamba raisi huyo si mzalendo,kwa vile tu ki-ujanja u-janja,alikwepa vita ya vietinamo, hili lilivuma zaidi wakati wa kampeni!
Sisi watanzania tunahitaji "upiganaji" kama ndio mizani ya kupima uzalendo wetu?si amini katika hilo.historia pia inaonesha mohheddali alinyang'anywa mkanda wa wba na jela aliiona,kwa vile aligoma kwenda vitani,robert nesta marley,ye alifurushwa toka u.s.
Hii kwa U.S mazingira yao wako sahihi,lakini hii si mizania sahihi kwa tanzania wala afrika kwa ujumla.
Vita zimepiganwa afrika na tanzania ikiwemo,lakini hata siku moja havijaleta neema kwa walio wengi,hivyo basi mapambano ya kivita si uzalendo,kama mwandishi wa kitabu cha mungu katika historia,Dk.Hanz,anavyo mnukuu marehemu Papa Paulo wa pili kwamba binadamu yupo karibu kuvuka mstari wa maangamizi kwake ye mwenyewe,na kwa sasa duniani hakuna binadamu aliye tayari kujiua.
Picha iliyo wazi ni kwamba vita haina nafasi kwa jamii "staarabu" kilicho baki ni kujiuwa mwenyewe,ambacho hakuna binadamu mwenye akili timamu anaye taka kufanya.
Tanzania inahitaji wazalendo,lakini si kutoka katika mstari wa mapambano,yenye dhana ya mtutu.ila ni kama vile profesa wa uchumi kutoka chuo kikuu cha ibadan,nigeria,t.ademola,anavyo andika kuhusu mabadiliko ya kiuchumi kupelekea kuondoa umaskini kwa wananchi wengi.hivyo uzalendo sahihi upimwa pale waliomadarakani wanapochukua maamuzi yanayo wanufaisha wengi katika kupambana na umasikini na ujinga na magonjwa,nasi vinginevyo.
Hata iwe vipi 'gwaride 'si njia ya kurudisha uzalendo.Wazalendo watalinda na kutetea maslahi ya nchi yao bila kutetereka,j.k.nyerere,nkurumah walipitia jkt gani iliyowapa moyo wa kizalendo katika kupambana na maadui ujinga,maradhi na uamasikini?hivyo si sahihi kama Miradji anavyo dai,kurejesha jkt;ili turejeshe uzalendo miongoni mwa kizazi cha 1980.
Kizazi kukosa uzalendo,ni kweli,lakini suala la kujiuliza ni,nini chanzo chake?kijarida fulani cha kidini,kinaandika ya kwamba ushawishi wa matendo ya kimaadili ya watendaji wa serikali walio madarakani ni msukumo 'tosha'kuelekea uzalendo-dumu miongoni mwa vijana.hii ni sahihi.
Ni ukweli uliowazi matendo ya watawala yanaweza kupelekea kujenga au kuufisha uzalendo.kizazi hiki kinacho tuhumiwa kukosa uzalendo kimezaliwa wakati wa madhila makubwa ya kiuchumi kutokana na vita ya Kagera.Kinauishi umasikini,kinaona haki za wengi zinavyopindishwa,utumiaji nguvu wa vyombo vya dola,wakulima wasivyo na mtetezi,shule bila walimu au vitabu,ndugu zao kukaa jela bila haki za binadamu kuheshimiwa,mali ya nchi kunufaisha wachache,kukosekana kwa ajira,ubovu wa barabara,kuporomoka kwa bei za mazao,ukosefu wa nafasi za masomo katika shule za serikali.Uoza wote huo unao wasonga hawana wa kuwatetea.
Walio madarakani wanashiriki katika kukandamiza tabaka la chini.mipango ya kiuchumi isiyo leta neema kwa walalahoi inasimikwa,ripoti ya ADB(African Development Bank) ya 1994,inaonesha tanzania imeingia katika mabadiliko ya kupunguza wafanya kazi 50000,kwa miaka mitatu.wamekosa ajira,wataishi vipi,utajiju!!!!!
Wakulima wakaletewa dhana jeuri ya biashara huria,tanzania imeiridhia bila kuweka udhibiti wa serikali.wakulima wananyonywa hicho ni kilio kila siku,wazalendo wako wapi!
Huu ndio uzalendo,kuwauza ndugu zako kwa watega uchumi wa kimataifa kwa sababu tu,unaitwa mitaa ya downing kupata chai ya jioni au capitol hill!
Profesa Seith Chachage anahoji uhalali wa soko huria kwa Tanzania,ndani ya ripoti yake juu ya mwenendo wa zao la korosho katika mikoa ya kusini mwa Tanzania.katika mfumo huu jeuri wa soko huria;huwezi kukiri kwamba viongozi wetu ni wazalendo hata kidogo.
Uzalendo ni kulinda maslahi ya watu wako;ni kujitoa kwa dhati katika kuwaletea maendeleo chanya.uzalendo ni kupambana na maadui njaa;ujinga na umasikini kwa njia sahihi.matendo ya viongozi ni mbegu kuelekea kuujenga au kuubomoa uzalendo;na si "gwaride"vitendo vya haki huamsha uzalendo,sasa tuuamshe.

Mabilioni ya 'JK' yamekosea njia

Habari za manung'uniko ya wafanyabiashara wadogo wadogo na wajasiriamali zinasikika nchi nzima na kupamba magazeti ya kila siku na habari katika televisheni. Katuni nazo zinachorwa kuonesha kinacho wakumba wananchi wa Tanzania juu ya kile walichoahidiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika mapango wa kuwawezesha watu masikini nchini katika kujipatia mikopo ili kujikwamua na hali ngumu ya maisha.

Ni wazi kuwa nia ya fedha za 'JK' ni nzuri ila awamu hii tena ingawa Rais anajua na watanzania wengi wanajua kuwa Benki si rafiki wa watu masikini lakini ndiyo wamepewa mabiloni hayo wayasimamie. Sijui ni nini kimefanya fedha hizi zilizo na ni ya kuwainu watu masikini zipelekwe benki ya CRDB na NMB huku ukweli huo juu ya masharti magumu ukiwa wazi kwa kila mtu pamoja na JK mwenyewe!

Hakuna anayeweza kusema ni watu wangapi mpaka sasa wameweza kukopa kwani takwimu zinazotolewa zinaonesha wazi kuwa masharti yamewashinda wakopaji walio wengi.

Rai za wahariri wa magazeti mbalimbali nchini yamewahi kujoji na yanaendelea kuhoji juu ya nani hasa alikuwa anastahili kupata mkopo huu. Hakuna anayetoa jibu kati ya wahusika wakuu yaani Serikali na Benki zenye dhamana ya kusimamia mabilioni hayo.

Kinachoonekana sasa ni kuwa wenye nacho ndiyo watakao ongezewa. Yaani hao watu katika waombaji idadi ya maelfu kupata watu wasiozidi ishirini katika tawi la NMB Bukoba ni ushahidi kuwa wakopaji waliowengi hawawezi kuyafikia mabilioni haya.

Mkoani Tanga vyombo vya habari wiki iliyopita viliripoti juu ya kuvunjika kikao kufuatia wawakilishi wa benki kukosa majibu ya hoja kadhaa toka kwa wajumbe wa chama mkoani humo waliotaka kufahamu juu ya muenendo wa ukopeshaji.

Sasa jamii ya kitanzania hailewei kulikoni? Hasa watu masikini waliokuwa wameweka tegemeo lao katika mabilioni haya ya JK. Ni wazi kuwa mabilioni haya si sadaka na ni lazima yalindwe ili kuhakikisha yanarudi tena ili kuweza kukopesha wengine.

Ila Benki hazikustahili kupewa dhamana ya kuendesha mkopo huu.Makala haya itajaribu kuonesha ni kwanini tunasema Benki kupewa mabilioni ya JK ni kukosea njia.

Mkopaji awe mdogo au mkubwa si tu hukopa sehemu yoyote ile bali ile aliyoizoea. Mfano mzuri ni wewe mwenyewe msomaji wangu nina hakika umewahi kukopa hivyo basi katika kukopa kwako haujawahi hata siku moja kukopa iwe bidhaa au huduma mahali usikowahi kununua hata siku moja.

Hicho ndicho kinachotokea kila siku kwa wafanyabiashara,ukimueleza kama ataweza kukukopesha atakwambia we si mteja wangu. hapa maana yake ni kwamba kama angekuzoea na mazoea hayo ni kuwa uwe unapata huduma kwake ndipo ataweza kukuamini.

Sasa Benki nchini si wakopeshaji wa watu masikini na watu wasio na dhamana leo hii unapowapa taasisi hizi ambazo hawajazoea kidili na watu masikini utegemee nini kama siyo watu wengi kunyimwa mikopo hiyo kama hali inayotokea sasa. Hili liko wazi.

Tusidanganyike na majina kwani kuitwa national Microfinance Bank, si wekli kuwa inajihusiha na watu masikini hata kidogo.

Ni wazi kuwa Benki hizi hazina uzoefu wa kujihusihsa na watu wenye mitaji midogo na hasa masikini.Hivyo basi kukosa uzoefu huu kumewafanya wawe mwiba wakati wote.

Inawezekana kuwa wao si wabaya lakini NMB na CRDB wangekuwa tu wakweli na waungwana kwa kukataa kundesha zoezi hili kwani ni wazi kuwa wao hawana mazoea ya kukopesha watu amsikini hili liko wazi.Sasa sijui ni nini kimewafanya waje katika kona ambayo wao hawana uzaoefu nayo?

Tazania kuna taasisi zenye uzoefu wa kukopesha watu wenye kipato kidogo. Lakini safari hii hawakuwpewa nafasi hii.Binafsi nina amni kwani tafiti mablimbalim zilizofanywa zinaonesha ataasisi hizi za kibanafsi ziznfanya vizuri na zinamulekeo kweli ule wa Grameen Benki ya Profesa Mohammed Yunus mshindi wa tuzo ya Nobel na raia wa Bangladesh.

Taasisi hizo nim akama PRIDE(T),SEDA,MEDA,FINCA na FEDA kuzitaja kwa uchache.lakini pupa ndiyo tuakpeleka mbalioni NMB na CRDB huku tukijua wzi kuwa si rafiki wa masikini.

Taasisi hizi zinzendesha shughuki zake karibia nchi nzima na mahali kote zinafanya kwa ufanisi has katika kuota mikopo kwa watu wenye kipato kidogo ambao ndiyo walemngwa wa mkopo wa JK.

Profesa wa Uchumi Leonard Shio na Divina Shio katika tafiti yao; Institutions and Performance of Micro Enterprise in Tanzania,ilibaini kufanya vizuri kwa PRIDE(T),MEDA,SEDA,FEDA katika miko ay Mbeya,Arusha na Moerogoro na wakopeshwaji walikuwa ni wafanya bisahra wadogo. Mabo elo hii wanapigwa dnadana na NMB na CRDB.Ekwli wa mabo ni9 kuwa Benki hizi hazina uzoefu wa kujihushishan an kutoa mikopo kwa waut masikini isipokuwa wamaedandia tu!

Tafiti fualani iliyyofanywa na Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu Mzumbe Josephat Itika aktika mji wa Morogoro ikihusianisha ushiriki wa wa Pride aktika kutoa amikopoo ana ukuaji wa ujasriamali,ilibaini kuwa PRIDE wana uwezo mkubwa wa kukusanya marejesho kwa zaidi ya 90% huku ikijikita kuwawezesha zaidi watu walio na kipato cha chini.

Lenye kutia moyo zaidi ni kuwa wakopaji wengi walikuwa ni akinam mama kwa zaidi ya 54%. Ni wazi kuwa mabilini haya ya JK kwa sasa yanatoka bila hata kujali usawa wa jinsia kitu ambco ni hatari.

SEDA(Small Enterprise Development Institute) ambayo ipo zaidia aktika mikopo aya kasiakazini mwa nchi mkoai Arshu pekee iliweza kukopesha watu zaidi ya 3000 wengi wao ndiyo hao Rais aliwalenga.

Pai taasisii hizi hutoa elimu kabla ya kutoa mikopo kwa wakoapji wake; juu ya namana ya kunedesha biashara kwa mafano PRIDE wana taasisi inayoitwa REDI. Ni wazi kuwa kama kusingekuwa na 'ushabiki' taasisi hizi zingekuwa ni za kupewa kundesha mkopo badala ya ahali ilivyo sasa.

NI wazi kuwa CRDB na NMB si taasisi zilizo na uzoefu wa kudili na watu wenye kipato kidogo. hatujachelewa kwani hadi sasa ni bilino 11 tu ndyo zimengizwa katika Benki hizo,na ni kiasi kidogo tu kimetoka. Ni bora kama tukiwapa kazi hiyo hizi taasisi zenye uzoefu wa kujishighulishs na watu masikini kama kweli tuna nia ya kuona umasikini wa kipato unapungua nchini.Na taasisi hizo ni PRIDE,MEDA,FEDA na zinginezo kuliko hali ilvyo sasa ya kuona tu mchezo wa maigizo.

Tukijipanga inawezekana kuwapa mitaji watu masikini lakini si kwa kupitia CRDB wala NMB.

Saturday, April 18, 2009

Muhogo zao linalohitaji msukumo mkubwa

Muhogo zao linalokumbukwa wakati wa njaa,halina thamani. Nakumbuka ukiwa shule ukionekana unakula muhogo’chipsi dume’, ilikuwa unataniwa kuwa utagombana na nguruwe. Duniani zaidi ya tani milioni 202.65 huzalishwa kila mwaka, na likitoa ajira kwa watu zaidi ya milioni 500, huku likitemegewa kama chakula kwa watu zaidi ya milioni 800 ulimwenguni kote.

Tanzania inakadiriwa kuzalisha zaidi ya tani milioni 2 za muhogo kwa mwaka..Tafiti nyingi zimefanywa na zinaendelea kufanywa zikijikita katika kufanya zao la muhogo kukubalika miongoni mwa jamii za watu masikini kuwa si kimbilio la njaa bali ni chakual bora na chanzo cha pato muhimu kwa wakulima wetu.. Pesa zinaungua na zitaendela kuungua katika kufadhili tafiti za moja kwa moja na tafiti za kichunguzi.

Hakuna ubaya katika kufanya tafiti, lakini wakati umefika tujiulize,je tunahitaji tafiti zaidi juu ya muhogo, na kama ndiyo katika maeneo gani hasa ambayo yanaleta vikwazo kwa zao hili.

Ili tuwe na uhakika lazima tujue masaibu yaliyolikumba zao hili hadi kufikia kusahaulika na kuonekana kuwa halina thamani nchini hadi njaa itokee, ndiyo utasikia pandeni mazao yanayostahimili ukame kama muhogo, loh siku zote tulikuwa wapi! Ukiangalia kwa haraka utaona ni Tanzania tu ndiyo zao hili liko nyuma na halithaminiwi miongoni mwa wananchi wake. Linalotia uchungu jamii inayokataa kula muhogo si kama ni zenye neema la hasha mara zote ni watu wakulilia misaada na fadhila za serikali au wahisani.

Wakulima wengi wanaolima muhogo nchini hufanya ni kama kilimo cha kujikimu, utatembelea maeneo ya vijijini utashangaa kujionea mashamba ya muhogo yamelaa miaka zaidi miwili bila kuvunwa ilihali ni chanzo cha kipato kwao. Lakini nchi za Africa magharibi muhugo ni lulu na unaingiza chumo zuri miongoni mwa wakulima wa nchi hizo.Haya hayakutokea tu ghafla bila mipango madhubuti.

Mfano katika Nigeria ni sera nzuri zilizofanya muhogo kuhimarika na kuwa chanzo cha pato miongoni mwa wakulima wake. Katika kila uzalishaji wa unga utokanao na nafaka miongoni mwa wazalishaji wakubwa wanatakiwa kutumia 5% ya unga wa muhogo. Hili hufanya mahitaji wa muhogo kuwa makubwa katika viwanda vya ndani vya usindikaji wa nafaka na kupelekea soko la uhakika.

Hivi karibuni nchini kupitia vyombo vya habari tumesikia kilio cha wadau wa zao la muhogo katika kuiomba serikali kufanya zao la muhogo kuwa la biashara. Kilio hiki si kipya ni cha muda mrefu na napenda kuweka wazi kuwa kufanya zao la muhogo kuwa ni zao la biashara ni kwa kulitafutia namna ya kupata soko la uhakika kwa kutunga sera endelevu zilizojikita katika tafiti na maendeleo (R&D). Tahadhari uuzwaji wa muhogo usifanywe kwa ajili ya kuchangaya kwa chakuala cha wanyama nchi yetu haijafikia huko.

Pamoja na kupigiwa debe kuwa muhogo unahitaji kuwa na soko la uhakika, ni wazi kuwa tahadhari inahitajika katika uandaaji wa zao hili kwa ajili ya chakula cha binadamu, kwani liliowazi ni kwamba muhogo ukiandaliwa vibaya unamadhara makubwa kwa binadamu kama vile kupooza kwa miguu kunachongiwa kwa kiasi kikubwa na uzalishaji wa mihogo michungu yenye sumu ya cyanogenic.

Tafiti zinaonesha hiki si kikwazo kikubwa kwa vile muhogo ukilowekwa katika maji kiasi hiki cha sumu hupungua, au hata ukianika juani kuna kiasi hupungua. Hizi ni habari njema na zenye kutia moyo katika kuona muhogo unavuka kigingi cha kuwa na sumu inayoweza kufanya miguu ya mtumiaji kupooza.

Kigingi kilichobaki kwa sasa katika kufanya muhogo uenda sokoni na kukubarika miongoni mwa jamii ya kitanzania ni sera na mtizamo wa kifikira. Mitizamo yetu hasi inatufanya tuwe watu wa kulia njaa kila wakati.

Bila kubadili mitizamo yetu katika milo siku zote tutakuwa ni watu wa kuona njaa inatunyemelea kisa mahindi hatukuvuna kiasi cha kutosha. Tunajaza watoto wetu fikira za woga kuwa akila muhogo ataonekana mchovu ni kandamizi na hasi kwa vizazi vijavyo vya nchi hii.

Mbunifu wa ‘corn flakes’ Dr John Harvey Kellogs na ndugu yake Will Keith Kellogs mwaka 1906 walifanyaubunifu nchini Marekani walitumia ngano nyeusi ambayo ilikuwa haithaminiwi kwa walaji na baada ya kuibadili kuwa hizo corn flakes ambazo leo hii ukienda supermarket kubwa duniani kote zinagombaniwa asili yake ni ngano nyeusi zilizodharauliwa na walaji. Na sisi tunaweza kubadili muonekano hasi wa zao la muhogo nchini.

Lazima tubadilike kwanza kifikra dhidi ya muhogo, na hakuna mchawi mwingine wa njaa inayotukumba ni kujaribu kufikia nadharia ambazo kitaalamu ni ndoto. Utashangaa mtu anakomaa kulima mahindi maeneo ambayo mvua ni haba, kisa chakula kikuu (staple food), ili iwe nini? Lima muhogo uone utapata nini?Muhogo unastahimili ukame hili lipo wazi.

Sera imara zenye kuona muhogo unafika sokoni zitasadia nchi hii. Muhogo unachangia zaidi ya asilimia 15 ya fuko la chakula kwa mwaka , na inawezekana kuongezeka endapo wakulima wataona kuwa kuna mtetezi wa kudumu, na utetezi huo si wa maneno bali sera kama zile za Nigeria. Tafiti zimefanywa nchini katika kuona uchanganyaji wa muhogo hauthiri ladha na muonekano wa vyakula vingine kama vile chapati, biskuti,maandazi na kadhalika.

Asilimia 25 ya unga wa muhogo inahitajika katika kutengeza maandazi. Sasa maandazi mangapi yanatengezwa kwa siku nchini, unga wa ngano tani ngapi unauzwa na kampuni zetu kila siku nchini.Muhogo ni lulu tubadilike.
E-mail fagdas1980@yahoo.com