Monday, April 20, 2009

Gwaride si njia sahihi ya kuleta uzalendo ila matendo ya watawala

Nimesikia na ninaamini umeshawahi kusikia watu wakieleza au kwa ukali au upendo neno "uzalendo".Imefikia hatua wengine katika mzungumzo ya kawaida kuwaita wenzi wao ni wa-zalendo au si wa-zalendo.Mimi najiuliza "uzalendo" ni nini?Mzalendo ni nani ?Ufanye nini ili uwe mzalendo?
Hata hao wanao wavua wenzao huo uzalendo,mara nyingi huwa hawana tafsiri isiyo na utata juu ya neno hili,uzalendo!Inashangaza sana.Ukiangalia sana kuna watu wengi,tia ndani wasomi ambao kwa wakati tofauti,wanaulezea huo uzalendo kama ni "hali".Hapa wanajenga picha ya kufikirika tu,au ni dhana tu ambayo inaweza kutofautiana kwa mchango wa mazingira yanayo mzunguka mtu mmoja toka sehemu moja hadi nyingine.
Kama tukikubali uzalendo ni hali,ni vipi sasa tunafamu mtu fulana ameikosa hiyo hali?Kwangu mimi vitendo hunena,basi matendo huonesha hali ya mtu kuelekea uzalendo,kama hivyo ndivyo basi,nakubali kwa dhati sasa kuingia kwenye "swimming pool" yenye maji kwa kujaribu kutoa tafsiri ya uzalendo.
'Uzalendo' ni ile hali ambayo binadamu anaihisi juu ya mashaka,taabu,shida,sononeko,hofu,madhara,inayo msibu yeye au mwenziwe,na binadamu hao kuwa na nia,malengo na makusudio ya kupambana na hali hiyo kandamizi kwa "gharama" sahihi kupelekea ushindi-dumu.sasa kama msingi mkubwa wa uzalendo ni mapambano sahihi,ili kupelekea faraja kwa walio na hali dhalili,je Afrika kuna wazalendo wa-kweli?
Dhana nyingine kubwa inayo jificha nyuma ya uzalendo ni mabadiliko,kuhusu mabadiliko,uzalendo unaamini ili mabadiliko yawe ya kizalendo lazima yawafaidi watu wengi hasa wa tabaka la chini,nao ni "wakulima"je mabadiliko ya kiuchumi na kijamii na kisiasa yanato tokea tanzania ni ya kizalendo?
Kuna wanao dai,kizazi cha sasa hasa walio zaliwa kuanzia miaka ya 1980,kimekosa uzalendo!Miradji mwandishi wa makala katika kona ya Darubini ya jumapili katika gazeti la majira la tarehe 26/9/03,anaunga mkono wazo kwamba kizazi cha sasa hakina uzalendo.
Kibubusa kabisa anasema JKT lirudishwe ili kurejesha huo uzalendo!je uzalendo ni kupiga "kwata".hata kidogo.
Nimeshaandika kwamba dhana ya uzalendo inaenda sambamba na mazingira,kwa mfano kwa nchi ya marekani,vita ni njia moja wapo ya kuonesha fulani ni mzalendo.wapinzani wa bush jr,walidai wazi kabisa kwamba raisi huyo si mzalendo,kwa vile tu ki-ujanja u-janja,alikwepa vita ya vietinamo, hili lilivuma zaidi wakati wa kampeni!
Sisi watanzania tunahitaji "upiganaji" kama ndio mizani ya kupima uzalendo wetu?si amini katika hilo.historia pia inaonesha mohheddali alinyang'anywa mkanda wa wba na jela aliiona,kwa vile aligoma kwenda vitani,robert nesta marley,ye alifurushwa toka u.s.
Hii kwa U.S mazingira yao wako sahihi,lakini hii si mizania sahihi kwa tanzania wala afrika kwa ujumla.
Vita zimepiganwa afrika na tanzania ikiwemo,lakini hata siku moja havijaleta neema kwa walio wengi,hivyo basi mapambano ya kivita si uzalendo,kama mwandishi wa kitabu cha mungu katika historia,Dk.Hanz,anavyo mnukuu marehemu Papa Paulo wa pili kwamba binadamu yupo karibu kuvuka mstari wa maangamizi kwake ye mwenyewe,na kwa sasa duniani hakuna binadamu aliye tayari kujiua.
Picha iliyo wazi ni kwamba vita haina nafasi kwa jamii "staarabu" kilicho baki ni kujiuwa mwenyewe,ambacho hakuna binadamu mwenye akili timamu anaye taka kufanya.
Tanzania inahitaji wazalendo,lakini si kutoka katika mstari wa mapambano,yenye dhana ya mtutu.ila ni kama vile profesa wa uchumi kutoka chuo kikuu cha ibadan,nigeria,t.ademola,anavyo andika kuhusu mabadiliko ya kiuchumi kupelekea kuondoa umaskini kwa wananchi wengi.hivyo uzalendo sahihi upimwa pale waliomadarakani wanapochukua maamuzi yanayo wanufaisha wengi katika kupambana na umasikini na ujinga na magonjwa,nasi vinginevyo.
Hata iwe vipi 'gwaride 'si njia ya kurudisha uzalendo.Wazalendo watalinda na kutetea maslahi ya nchi yao bila kutetereka,j.k.nyerere,nkurumah walipitia jkt gani iliyowapa moyo wa kizalendo katika kupambana na maadui ujinga,maradhi na uamasikini?hivyo si sahihi kama Miradji anavyo dai,kurejesha jkt;ili turejeshe uzalendo miongoni mwa kizazi cha 1980.
Kizazi kukosa uzalendo,ni kweli,lakini suala la kujiuliza ni,nini chanzo chake?kijarida fulani cha kidini,kinaandika ya kwamba ushawishi wa matendo ya kimaadili ya watendaji wa serikali walio madarakani ni msukumo 'tosha'kuelekea uzalendo-dumu miongoni mwa vijana.hii ni sahihi.
Ni ukweli uliowazi matendo ya watawala yanaweza kupelekea kujenga au kuufisha uzalendo.kizazi hiki kinacho tuhumiwa kukosa uzalendo kimezaliwa wakati wa madhila makubwa ya kiuchumi kutokana na vita ya Kagera.Kinauishi umasikini,kinaona haki za wengi zinavyopindishwa,utumiaji nguvu wa vyombo vya dola,wakulima wasivyo na mtetezi,shule bila walimu au vitabu,ndugu zao kukaa jela bila haki za binadamu kuheshimiwa,mali ya nchi kunufaisha wachache,kukosekana kwa ajira,ubovu wa barabara,kuporomoka kwa bei za mazao,ukosefu wa nafasi za masomo katika shule za serikali.Uoza wote huo unao wasonga hawana wa kuwatetea.
Walio madarakani wanashiriki katika kukandamiza tabaka la chini.mipango ya kiuchumi isiyo leta neema kwa walalahoi inasimikwa,ripoti ya ADB(African Development Bank) ya 1994,inaonesha tanzania imeingia katika mabadiliko ya kupunguza wafanya kazi 50000,kwa miaka mitatu.wamekosa ajira,wataishi vipi,utajiju!!!!!
Wakulima wakaletewa dhana jeuri ya biashara huria,tanzania imeiridhia bila kuweka udhibiti wa serikali.wakulima wananyonywa hicho ni kilio kila siku,wazalendo wako wapi!
Huu ndio uzalendo,kuwauza ndugu zako kwa watega uchumi wa kimataifa kwa sababu tu,unaitwa mitaa ya downing kupata chai ya jioni au capitol hill!
Profesa Seith Chachage anahoji uhalali wa soko huria kwa Tanzania,ndani ya ripoti yake juu ya mwenendo wa zao la korosho katika mikoa ya kusini mwa Tanzania.katika mfumo huu jeuri wa soko huria;huwezi kukiri kwamba viongozi wetu ni wazalendo hata kidogo.
Uzalendo ni kulinda maslahi ya watu wako;ni kujitoa kwa dhati katika kuwaletea maendeleo chanya.uzalendo ni kupambana na maadui njaa;ujinga na umasikini kwa njia sahihi.matendo ya viongozi ni mbegu kuelekea kuujenga au kuubomoa uzalendo;na si "gwaride"vitendo vya haki huamsha uzalendo,sasa tuuamshe.

No comments: